Mfumo mpya Wa afya data Kuwaanufaisha Wafugaji nchini

September 1, 2017

Happy Lazaro, mwananchi mwananchipaper@mwananchi.co.tz

Arusha. Jamii ya Waf ugaji waishio Wilayani Ngorongoro mkoani Arusha Wamenufaika na mfumo mpya wa afya data unaowaWezesha kutuma taarifa Za dalili ya magonjwa ya Wanyama, binadamu kupitía simu za mkonomi na kupata mrejesho kwa Wakati.

Akizungumza kuhusiana na mfumo huo, mkuu wa Kituo cha Umahiri cha Afrika (SACIDSACE), Profesa Gerald Misinzo allisema lengo la kuanzisha mfumo huo ni kuboresha afya ya mifugo na Wanyama katika bara la Afrika. Alisema kuwa mfumo huo unawawezesha jamii hiyo ya Wafugaji kutoa taarifa ya magonjwa kwa wanyama pamoja na binadamu kuzituma kwa Wataalamu ili kupata mrejesho kwa haraka na hatimaye kuchukua tahadhari Mapema. .

Profesa Misinzo allise la kuwa mfumo huo umeanzishwa na kituo cha utafiti na ufuatiliaji Wa magonjwa ambukizi kilichopo kusini mwa bara la Afrika ambako mifumo hiyo imeunganishwa kupitia simu za mkonOni na imeWekWa katika maeneo li yenye wafugaji wengi kwa kuwa ndiko magonjwa ya milipuko yanapoanzia.

Alisema kuWa maeneo mingine yaliyonufaika na mfumo huo ni pamoja na Mkoa Wa Morogoro, Wilaya ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Dar es. Salaam ambapo kwa wilaya ya ngorongOro tayari WametOa mafunzo kwa Wataalamu 33 ambao Simu zao zimeunganishwa na mfumo na ndiyo Wanaofanyakazindaniyajamii inayowazunguka.

“Si Si tumeamua kusaidia jamii hizo za wafugaji ili Waweze kuripoti taarifa zao Za Wanyama na binadamu kwa wataalamu hao na kupata mrejesho kwa wakati na mfumo huu umatuwezesha kugundua matatizo hayo mapema na kuchukua tahadhari na kuepuka gharama katika kutibu” allisema.

Share on FacebookTweet about this on TwitterShare on LinkedInShare on Google+Email this to someone