SACIDS YAPONGEZWA KWA KUBUNI MFUMO WA MAWASILIANO WA KIDIJITALI

February 17, 2017

Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya wanyama na binadamu Kusini na Mashariki mwa Afrika, (SACIDS), imepongezwa kwa kubuni mfumo wa Mawasiliano ya kidijitali ya kubaini, kutoa taarifa mapema na kuchukuliwa hatua za kutibu tatizo kwa haraka.

Pongezi hizo zimetolewa na Kaimu Naibu wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,SUA, Prof. Patrick Mwang’ingo alipokuwa akifungua mkutano wa uwasilishaji taarifa za utafiti unaofanywa na taasisi ya SACIDS inayofanya shughuli zake katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, mkutano uliofanyika mjini Morogoro nchini Tanzania.
Prof. Mwang’ingo amesema mfumo huu wa Mawasiliano kwa njia za kidijitali utarahisisha lengo la SACIDS la kutoa taarifa mapema na kutafuta na kutekeleza kwa wakati suluhisho la tatizo husika kwa kuwatumia maripota maalumu kutoka vijijini kutoa taarifa mapema.
Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Prof. Mark Rweyemamu alisema lengo la mradi ni kufikia hatua ambayo Afrika yenye Afya inafikiwa na kwa kutumia utaalamu wa Mawasiliano ya kidijitali ambapo Jamii ikiwa hukohuko vijijini itasema tatizo na wataalamu watashughulikia kwa haraka.
Share on FacebookTweet about this on TwitterShare on LinkedInShare on Google+Email this to someone