Tamko Kuhusu Taarifa ya Ugonjwa wa Ebola Katika Nchi Jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

May 16, 2017

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepata taarifa kupitia “International Health Regulations – National Focal Point” kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ulio tangazwa na Shirika la Afya Duniani siku ya tarehe 12 Mei, 2017. Ugonjwa wa Ebola umethibitishwa kwa kupitia vipimo vya maabara baada ya kutokea wagonjwa 9, ambapo kati yao 3 walipoteza maisha na wengine sita (6) wanaendelea na matibabu katika kituo kilichoandaliwa. Ugonjwa huo umetokea katika Jimbo la North-east BasUele linalopakana na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

TAMKO TAHADHARI YA EBOLA
Share on FacebookTweet about this on TwitterShare on LinkedInShare on Google+Email this to someone